Monday, January 9, 2012

TAARIFA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA
ASKARI WA WANYAMAPORI AMEUWAWA NA MAJANGILI KATIKA PORI LA AKIBA LA MASWA
Wizara ya Maliasili na Utalii inasikitika kutoa taarifa kwa umma kuwa tarehe 03/01/2012 mnamo saa 6.20 usiku, askari wa Wanyamapori aitwaye Dorcas K. Rumbagi alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili katika Pori la Akiba la Maswa. Marehemu alifariki njiani alipokuwa akipelekwa hospitali.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda Kibara - Bunda mkoani Mara ambako alizikwa tarehe 6/01/2012.

Taarifa kuhusu kitendo hicho cha mauaji ya askari wa wanyamapori ilitolewa katika Kituo cha Polisi cha Meatu na hadi sasa watuhumiwa kumi wameshakamatwa na wanaisaidia polisi.

Wizara inachukua fursa hii kuwaomba wananchi wanaoishi karibu na Pori la Akiba la Maswa, na sehemu zingine, kutoa ushirikiano ili waliohusika wote na mauaji hayo waweze kukamatwa.

Wakati huohuo Wizara imeongeza askari katika Pori la Akiba la Maswa ili kuimarisha ulinzi.


George Matiko

MSEMAJI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

No comments: