Thursday, February 16, 2012

BASI LA HAPPY NATIONAL LAPATA AJALI MKOANI MBEYA
Basi
la Happy Nation limeanguka baada ya kushindwa kuumudu mteremko wa
TAZAMA, maarufu kama Pipeline. Habari toka kwa abiria waliopanda basi
la Nganga, anasema watu wamejeruhiwa vibaya ila hakuna vifo. Basi hilo
likiwa kwenye mwendo kasi lilitaka kulipita basi la Nganga, lakini
kukawa na gari jingine linapandisha mlima huo, ndipo dereva akalazimika
kulirudisha nyuma ya basi la Nganga na kuligonga kwa nyuma na kupinduka.
Abiria wa basi la Nganga wamesalimika wote.

picha na Felix Mwakyembe

No comments: