Wednesday, February 22, 2012

DKT. SHEIN AONGOZA UZINDUZI WA MAULID KISIWA CHA TUMBATU ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dk, Ali Mohamed Shein akisalimiana na Masheikh na waheshimiwa mbalimbali alipohudhuria katika Kisiwa cha Tumbatu Zanzibar kwa ajili ya kuzindua Maulidi ya Kusherehekea kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW).
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akielekea katika sehemu aliyotaharishiwa kwa ajili ya Uzinduzi wa Maulidi hiyo Kisiwa cha Tumbatu Zanzibar.
Rais wa Zainzibar Dk Ali Mohamed Shein (watatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na Masheikh na Viongozi mbalimbali waliohudhuria Uzinduzi wa Maulid ya kusherekea kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) katika kisiwa cha Tumbatu Zanzibar.
Uzinduzi wa Maulidi Huenda sambamba na kupandishwa Bendera ya Dini kama Ishara ya kusherehekea kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW).
Sheikh Othman Maalim akitoa mawaidha katika Uzinduzi wa Maulid ya kusherekea kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) katika kisiwa cha Tumbatu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akiwahutubia Waislamu na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Msikiti mkuu wa Tumbatu Zanzibar alipozinduwa Maulidi inayofanyika kila mwaka kisiwani humo.PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI - MAELEZO ZANZIBAR.

No comments: