Wednesday, February 22, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA DAHARIA LA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA KORONGWE BEACH-WILAYA YA NKASI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kushoto kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akinawa maji ya Kisima cha kupampu yanayovunwa kwa mvua, kilichojengwa katika Kijiji cha Mwamapuli wakati alipokuwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi juzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkazi wa Kijiji cha Mwamapuli, Yacoub Jilala, ambaye ni mlemavu, baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho, alipofika kuzindua jengo la Ghara la mazao, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi, juzi Februari 20, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu nje ya jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, baada ya kuzindua Daharia hilo wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Nyuma yake ni mkewe Mama Asha Bilal na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Korongwe kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi jana Februari 21, 2012.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments: