Kamanda Misime wa kanda ya kipolisi Wilaya ya Temeke akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kusimamia zoezi la kuzima moto katika kiwanda cha magodolo cha Pan African kilichopo Chang'ombe jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kimeteketea kabisa kwa moto kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mashine za kunolea visu vya kukata magodolo kiwandani hapo, Kamanda Misime amesema hakuna taarifa ya mtu yeyote kupoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo la moto
Magari ya vikosi vya kuzima moto yakiwa yamejipanga katika kiwanda hicho yakiendelea na kazi ya kuzima moto.
Picha na John Bukuku wa FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment