Friday, February 3, 2012

Mahafali Korogwe Girls yageuka vilio na simanzi Jana

Mmoja wa majeruhi waliogongwa na gari lenye namba T489 AGJ aina ya Toyota Bw. Elias Ngole almaarufu Ngoswe ambaye ni mpiga picha maarufu mkoani Tanga, aliyefika kwenye mahafali ya kidato cha sita katika shule hiyo ya Korogwe Girls akiwa amepakiwa kwenye bajaj kukimbizwa katika hospitali ya magunga kwa matibahu
Mkuu wa wilaya ya Korogwe (mwenye suti nyeusi) akiwa amemshika mwanafunzi Kibibi Mmasa (19) ambaye ndiye anayetuhumiwa kuendesha gari hilo kwa kuliweka gea kisha gari hilo kurudi nyuma na kuwagonga wanafunzi wenzake na kuwasababisha majeraha makubwa mwilini.
Mwanafunzi Renata Renatus anayesoma kidato cha sita katika shule hiyo, akiwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe akihudumiwa na muuguzi alipofikishwa katika hospitali hiyo.

Gari lenye namba T 489 AGJ likiwa limesimama katika eneo la shule baada ya kutuhumiwa kuwagongwa wahitimu wa shule hiyo waliokuwa wamesimama wakisubiri sherehe za mahafali hayo.
Picha na Mashaka Mhando wa Globu ya Jamii, Tanga
Kwa Hisani ya Issa Michuzi Blog

No comments: