Friday, February 3, 2012

NAPE AKABIDHI MIFUKO 620 YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI WA MADARASA YA SHULE MUSOMA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akikabidhi mifuko 600 ya saruji kwa mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa, katika hafla iliyofanyika Ofisi ya mkuu huyo wa mkoa leo. Saruji hiyo ambayo ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari mkoani kuwezesha wanafunzi waliofaulu mwaka huu kupata vymba vya kusomea. Kulia ni makada wa CCM waliotoa msaada wa saruji hiyo. Mjumbe wa NEC, Vedastus Mathayo (mifuko 100), Mfanyabiashara Joseph 'Msukuma' Kasheku (mifuko 100) na Mfanyabiashara Zuffikar Nanji (mifuko 400).

NA BASHIR NKOROMO,MUSOMA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeukabidhi mkoa wa mara mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari mkoani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 35 ya CCM.

Saruji hiyo itatumika kujenga madarasa kwa ajili ya wanafunzi mkoani humo ambao wameshindwa kwenda sekondari kutokana na uhaba wa madarasa licha ya kufaulu mwaka huu kuanza kidato cha kwanza.

Akikabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa mkoa huo, John Tupa, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema mifuko 400 imetolewa na kada wa CCM Zulfikar Nanji wa Kampuni ya Mwanza Huduma Ltd na Mfanyabiashara Joseph 'Msukuma' Kasheku na Mjumbe wa NEC, Vedastus Mathayo ambao wote wametoa mifuko 100 kila mmoja.

Nape aliwashukuru wafanyabiashara makada hao wa CCM kwa kuiunga mkono CCM katika kuhakikisha kwamba sherehe za miaka 35 ya CCM inakuwa na mafanikio makubwa kwa kutekeleza azma ya kuchangia shughuli za maendeleo.

Alipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa alisema, jumla ya watoto 6486 kati ya asilimia 50.3 ya watoto waliofaulu, wapo nyumbani baada ya kukosa nafasi ya kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu baada ya kufaulu mwaka huu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa unahitaji madarasa 718 wakati yaliyopo ni 479 na hiyo kuwa na upungufu wa madawati239 na kwamba wilaya ya Bunda ndiyo inayoongoza kuwa upungufu wa madarasa.

Alisema licha ya kupata msaada huo wa saruji bado mkoa unahitaji mabati, mbao na madawati kwa ajili ya madarasa yatakayojengwa.

No comments: