Monday, February 6, 2012

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL APOKEA WANACHAMA WAPYA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA CCM KIBAHA VIJIJINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mafia, Abdallah Mdimu, baada ya Wilaya hiyo kuibuka mshindi wa kwanza kwa ulipaji wa Ada za Wanachama, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya chama hicho zilizofanyika Wilaya ya Kibaha Vijijini jana Februari 5, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kadi ya mwanachama mpya kutoka CUF, Omar Said Hunda, aliyeamua kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, zilizofanyika Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, jana Februari 5, 2012.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mohamed Shaban, akimbeba juu juu mwanachama mpya, Omar Said Hunda, aliyekuwa mgombea Udiwani Kata ya Dutumi kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi wa mwaka 2010, aliyejiengua katika chama hicho na kujiunga na CCM. Hapa mwanachama huyu alikuwa akipelekwa mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kukabidhi kadi yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, zilizofanyika Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, jana Februari 5, 2012.
Baadhi ya Wanachama wapya waliojiunga na Chama cha Mapinduzi CCM, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya chama hicho zilizofanyika jana Februari 5, 2012 Wilaya ya Kibaha Vijijini.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais


No comments: