Tuesday, February 14, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWASILI MKOANI RUVUMA KUANZA ZIARA YA SIKU NNE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma, Delphin Fredrick, ambaye ni mmojakati ya viongozi wa vyama vya upinzani waliohudhuria mapokezi ya Makamu wa Raisalipowasili mkoani Ruvuma leo Febriari 14,2012 kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku nne.Viongozi wengine wa Upinzani waliokuwapo ni pamoja na Katibu (W) Songea mjini wa Chama chaCUF, Mohmed Makoma, Katibu wa TLP Mkoa Ruvuma, Wellnery Methody Kilowoko na Mwenyekiti wa(W) Songea Mjini TLP, Elias Nchimbi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Thabit Mwambungu, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara yke ya siku nne leo Februari 14, 2012. Akiwa mkoani Ruvuma, Dkt Bilal atakagua
miradi mbalimbali ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi katika baadhi ya miradi ya mkoa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge Vita Kawawa, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mkoani Ruvumaleo Februari 14, 2012 kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku nne katika mkoa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akifurahia ngoma ya asili wakati wa mapokezi yake kwenya uwanja wa ndege wa mkoani Ruvumaleo Februari 14, 2012 alipowasili kwa ajili ya kuanza zizra yake ya siku nne mkoani humo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: