Tuesday, February 14, 2012

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP - OGP)
Tanzania imeridhia kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazri (Open Government Partnership – OGP). Mpango huu ni juhudi za kimatifa katika kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji wa huduma bora.
Vigezo vya nchi kuwa mwanachama wa Mapango huu ni pamoja na kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa (Country Action Plan) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na wananchi.
Kwa kuanzia, uandaaji wa utekelezaji wa Mpango huo utahusisha vipaumbele katika sekta tatu za Afya, Elimu na Maji ili kuimarisha uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika utoaji wa huduma.
Mpango huu sasa unaboreshwa kwa kupokea maoni na ushauri kutoka kwa Wananchi na Wadau mbalimbali. Njia za kukusanya maoni pamoja na Tovuti ya Wananchi (www.wananchi.go.tz), barua kupitia Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, S.L.P. 9120, Dar es Salaam, ujumbe bila malipo kupitia simu ya mkononi (SMS) namba 0658-999222, barua pepe: ogp@ikulu.go.tz.
Mpango Kazi wa OGP Tanzania unapatikana kwenye Tovuti ya Wananchi – www.wananchi.go.tz . Wananchi na Wadau wengine wanaimizwa kushiri kikamilifu kutoa maoni yao katika kuboresha Mpango Kazi wa OGP Tanzania. Mwisho wa kupokea maoni/ushauri au mapendekezo ni tarehe 30/03/2012.

IMETOLEWA NA OFISI YA RAIS
IKULU – DAR ES SALAAM
TAREHE:.14 Februari 2012.

No comments: