Thursday, February 2, 2012

MAKUBALIANO YA MKUTANO KATI YA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI NA ‘TASK FORCE’ YA MADAKTARI BINGWA WA MNH



1. TUMEKUBALIANA KUWA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA MADAI YA MADAKTARI NI
MOJA NA HAKUNA YEYOTE MWENYE MAMLAKA YA KUKUTANA, KUJADILI AU KUKUBALIANA NA SERIKALI JUU YA MADAI HAYO ISIPOKUWA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI AMBAYO INAJUMUISHA MADAKTARI BINGWA PIA KAMA WANAJUMUIYA.


2. TUMEKUBALIANA KUWA NA TAARIFA YA UPOTOSHAJI JUU YA MALENGO YA TIMU
HIYO YA MADAKTARI BINGWA, KIMSINGI LENGO LAO HASA ILIKUWA NI KUISHINIKIZA SERIKALI KUCHUKUA HATUA HARAKA ILI KUNUSURU HALI YA AFYA NCHINI.


3. PIA TUMEKUBALIANA KUWA KUTOKANA NA HALI YA UZOROTAJI WA HUDUMA YA
AFYA TUNATOA MWITO KWAMBA KAMATI KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MADAKTARI KUWA IPO TAYARI HATA LEO KUKAA NA SERIKALI MEZANI ILI KUFIKIA HITIMISHO YA MGOGORO HUU.


4. TUNGEPENDA SERIKALI KUACHA KUTOA VITISHO NA KUKAMATA NA KUWEKA
RUMANDE BAADHI YA MADAKTARI HAPA NCHINI. KITENDO HICHO HAKITOI SULUHU YA TATIZO HUSIKA.


5. MWISHO SERIKALI ISIJARIBU KUKWEPA KUWASILIANA NA KAMATI SABABU KAMA
KUNA NJIA YOYOTE YA KUFIKIA SULUHU YA TATIZO HILI NI KUPITIA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI.




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI IMEISHATOLEWA IKIWEMO STAR TV, ITV,
CHANNEL TEN, TUMAINI TV… MAGAZETI KAMA VILE THE CITIZEN, DAILY NEWS, JAMBO LEO, HABARI LEO, MWANANCHI NA KADHALIKA.


SOLIDARITY FOREVER

No comments: