Thursday, February 2, 2012

Rais Jakaya Kikwete Mgeni Rasmi Maadhimisho Ya Siku Ya Sheria Nchini

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Mahakama ya Rufaa Tanzania ,kuhusu siku ya sheria nchini itakayofanyika kesho jiji Dares Salaam.Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa Tanzania , Francis Mutungi.
baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kati yao na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (ambaye hayupo pichani ) kuhusu siku ya sheria nchini itakayofanyika kesho jijini Dares Salaam.
---


NA ZAWADI MSALLA- MAELEZO
2/2/2012
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini, yatakayo fanyika kitaifa katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema maadhimisho hayo yamelenga katika kujadili masuala mbalimbali ya kisheria ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi kwa ujumla.Jaji Mkuu aliongeza kuwa wananchi wengi wanapoteza haki zao za msingi kwa kutokujua sheria, hivyo kuna umuhimu wa kujua aina za makosa na adhabu zinazoweza kutolewa katika makosa hayo.
“Tangu kuanzishwa kwa sherehe hizi, zimelenga zaidi katika kuhakikisha wananchi wanajua mambo mbalimbali ya kisheria yanayowahusu kwani wengi huwa wanapoteza haki zao za msingi kwa kutokujua sheria, kutokujua sheria haina msamaha katika kosa.” alisema Jaji Mkuu.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni adhabu Mbadala katika kesi za Jinai: Faida zake katika jamii.
Shereha hizo pia zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Rais wa chama cha Mawakili nchini.


No comments: