Wednesday, February 8, 2012

MKUU WA MKOA WA MOROGORO ATEMBELEA SEHEMU YA UJENZI WA BWAWA LA KIDETE, WILAYANI KILOSA

Mhandisi Mshauri wa Kampuni ENV Ltd ya Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Fredrick Mtoga (kulia) akitoa maelezo mafupi namna walivyoweza kuuchepusha mto wa Mkondoa wakati wa ujenzi wa Bwawa la Kidete, Wilaya ya Kilosa, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (mwenye kaunda suti ) alipotembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo hivi karibuni.
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ENV Ltd ya Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Fredrick Mtoga (anayechora ardhini) akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa Bwawa la Kidete, Wilaya ya Kilosa, kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( mwenye Kaunda suti ) wakati alipotembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (mwenye Kaunda suti) akiongozana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mgeni Baruani ,(wapili mstari wa pili kutoka mbele) alipofanya ziara ya kuangalia mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidete , Wilaya ya Kilosa hivi karibuni.
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ENV Ltd ya Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Fredrick Mtoga (anayenyoosha mkono ) akionesha eneo ambapo mto wa zamani ulipokuwa ukipita kabla ya kuchepusha mto huo ili kutoa nafasi ya ujenzi wa Bwawa la Kidete, Wilaya ya Kilosa, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( mwenye Kaunda suti ) wakati alipotembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo hivi karibuni.Picha na John Nditi wa Blobu ya Jamii.
Na Issa Michuzi Blog

No comments: