Thursday, February 9, 2012

PINDA ANATAKA KUKUTANA NA MADAKTARI

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YUPO DAR ES SALAAM KUTOKA DODOMA KUSHUGHULIKIA MGOMO WA MADAKTARI AMBAO UMEKUWA UKIENDELEA KWA LENGO LA KUUPATIA UFUMBUZI. JANA AMEKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PAMOJA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA WASTAAFU. LEO SAA 3 ASUBUHI ATAKUTANA NA MADAKTARI BINGWA, MADAKTARI WALIOSAJILIWA (REGISTRALS) NA MADAKTARI WALIOKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS) NA BAADA YA HAPO SAA 4 ATAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD NA WAWAKILISHI KUTOKA HOSPITALI ZA MKOA WA DAR ES SALAAM, KWENYE UKUMBI WA CPL, MUHIMBILI. MATARAJIO YA SERIKALI NI KWAMBA MAZUNGUMZO HAYO YATAWEZA KUMALIZA MGOGORO HUU NA MADAKTARI WOTE KUREJEA KAZINI NA HIVYO KUREJESHA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HALI YA KAWAIDA KWA WANANCHI WA TANZANIA. HIVYO SERIKALI INAWAOMBA WOTE WANAOHUSIKA WAFIKE KATIKA MIKUTANO HIYO BILA YA KUKOSA.
(IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments: