Saturday, February 11, 2012

RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA WABUNGE WA CCM MJINI DODOMA.


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini kuzungumza na wabunge wa CCM katika kikao chake na wabunge hao kilichofanyika jana jioni Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.Wengine kutoka kushoto ni Spika wa Bunge Anne Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.


Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Muhagama akitoa maelezo ya awali kabla ya Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kuzungumza na wabunge hao. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara ) Pius Msekwa.


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wabunge wa CCM, katika kikao chake na wabunge hao jana katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.


Mbunge wa Simanjoro Ole Sendeka akitoa hoja zake katika kikao hicho.(Bashir Nkoromo).

No comments: