Wednesday, February 8, 2012

SHUKRANI ZA DHATI

Khadija Abdul - 1972 – 2012
SHUKRANI

Familia ya Ndugu Abdallah Mrisho Salawi - Meneja Mkuuwa Global Publishers Ltd, inachukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna mojaau nyingine, katika mazishi na maziko ya mpendwa mkewe, Khadija Abdulhussien,aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamis Feb 2, 2012, katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam.

Shukraniza pekee ziwaendee wafanyakazi wote wa Global Publishers na hususani MkurugenziMtendaji, Ndugu Eric Shigongo, ambaye alikuwa akifuatilia kwa karibu maendeleoya afya ya marehemu tangu mwanzo na kutoa ushauri kila mara, alijitolea kwahali na mali ili kuokoa maisha ya mpendwa wetu bila kuchoka hadi dakika yamwisho neno la Mungu lilipotimia.

Shukranipia ziwaendee Dk. Wayi wa Kinondoni Hospital, Dk. Hirji wa Ebrahim HajjiHospital na Dk. Nyawawa wa Aga Khan Hospital kwa jitihadi walizozifanya za kujaribukuokoa maisha ya Khadija.

Familiainawashukuru pia majirani, jamaa na marafiki wote wa Mrisho waliyoko nchini nanje ya nchi ambao wamekuwa wakimfarijikwa njia mbalimbali za mawasiliano na kumtia moyo katika kipindi hiki kigumu.

Familiahaina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombeakwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekeathawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budikumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (khadija) ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Mungu sote tutarejea!

Munguampumzishe Khadija katika moja ya viwanja vya peponi – Amen!

No comments: