Wednesday, February 8, 2012

Wanaharakati waandamana na kufunga barabara kwa muda jijini dar kuishinikiza serikali kumaliza tofauti zake na mgomo wa madaktari unaondelea nchini

Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Bi Helen Kijo-Bisimba akiwa na bango lenye ujumbe kwa serikali ukimtaka rais Jakaya Kikwete kuwafuta kazi mara moja Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr Haji Mponda, Naibu waziri wake Dr Lucy Nkya, katibu mkuu Blandina Nyoni na Mganga mkuu Dr Deo Mutasiwa kwa kushindwa kuzuia mgomo wa madaktari nchini.Aliyekaa katikati ni mkurugenzi wa Tamwa Ananilea Nkya na kushoto ni Anastazia Rugaba wa HakiElimu
Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Bi Helen Kijo-Bisimba akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusiana na wao (wanaharakati) kufunga barabara ya Ally Hassan Mwinyi na Ocean Road eneo la salander bridge jijini Dar es Salaam kwa muda ili kufikisha ujumbe kwa serikali kuhusu swala zima la mgogoro wa madaktari,na kubanisha lengo lao kuwaonesha watoa maamuzi kuwa hawaridhiki na hatua wanazochukua katika kushughulikia mgogoro wa madaktari
Mkurugenzi wa TAMWA,Mama Ananilea Nkya (kulia) akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mbalimbali kuhusiana na maandamano yao yaliyodumu kwa muda wa masaa mawili hivi kwa ajili ya kuishinikiza Serikali ikae meza moja na madaktari na kuhakikisha mgomo wao unakoma mara moja na kuhakikisha shughuli za matibabu hospitali ya Muhimbili na nyinginezo zinaendelea kama kawaida.
Amri ikitolewa kuwataka wanaharakati kuondoka eneo hilo,kwani ilielezwa kuwa maandamano hayo yamefanyika bila kubarikiwa.
Askari wakiwa eneo la tukio mapema leo jioni.
Ujumbe kutoka kwa wanaharakati hao.
Mwanaharakati akiwa na ujumbe wake.


Gari la askari ikihangaika kuchomoka kwenye mtungo uliosababishwa na maandamano ya wanaharakati mapema leo jioni.
Mtungo ukiwa umenoga mapema leo jioni uliosababishwa na maandamano ya Wanaharakati waliokuwa wakiandamana mapema leo jioni kuishinikiza Serikali kumaliza tofauti zake na madaktari ili kurudisha huduma za afya mahospitalini.Mgomo huo wa Madaktari umedumu kwa zaidi ya wiki moja sasa kutokana na msuguano na serikali,hali iliyopelekea kuzorota kwa huduma za afya sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali ya Taifa Muhimbili.
KWA HISANI YA JIACHIE BLOG

No comments: