Thursday, March 1, 2012

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MSHUJAA WA VITA VYA MAJIMAJI MJINI SONGEA
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiongea wakati wa Sherehe za
kumbukumbu ya Mashujaa wa vita ya Majimaji iliyoadhimishwa jana mjini
songea.Kushoto ni Kkatibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi
Maimuna Tarishi na Kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel Zullu.


Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara,Kanal Mstaafu Joseph Simbakalia akiongea na wakazi wa
Mkoa wa Ruvuma wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita
vya Majimaji yaliyofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini
humo.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi.
Maimuna Tarishi na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu.


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi akiongea na
wakazi wa manispaa ya songea kwenye maadhimisho ya kumbukmbu ya Mashujaa
wa Vita vya Majimaji mjini songea jana.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma,Mh. Said Mwambungu na kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel
Zullu.


Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiweka ngao na mkuki katika mnara
wa kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini songea


Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu,Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi,Mwenyekiti wa Baraza la
Wazee Mkoani Ruvuma,Alhaji Mustafa Songambele na Mkuu wa Zamani wa Mkoa
wa Ruvuma,Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo wakiinua mikono juu ikiwa
ni ishara ya kuomba dua kwa Mashujaa wa Vita ya Majimaji wakati wa
maadhimisho ya Mashujaa hao mjini songea jana.

No comments: