Monday, March 12, 2012

Rais Kikwete akiongea na Wazee wa Jijini Dar leo Kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Wazee wa Jijini Dar es Salaam wakati huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,ambapo hivi sasa anaongelea sakata zima la mgomo wa Madaktari.
 Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakifuatilia kwa makini Mkutano huo wa Rais Kikwete na Wazee wa Jijini Dar wa Salaam unaoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa pamoja na Mh. Iddi Simba wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Sehemu ya wazee wa jijini Dar es Salaam waliohudhulia kwenye mkutano huo na Rais Kikwete kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hivi sasa.Picha ni kwa Hisani wa TBC. 
Kupitia kwa Mtaa kwa Mtaa Blog

No comments: