Tuesday, April 10, 2012

BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA TIBA NA KUJITOLEA KUFANYA USAFI MAENEO YA HOSPITALI YA TEMEKE



 Mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, Zainabu Abbasi pamoja na mwanawe, Kheri Hasifu wakipokea boksi la sabuni ya kufulia kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Ilala, Gaudence Shawa, wakati wafanyakazi wa NBC walipofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na kushiriki shughuli za usafi jan. Kulia ni Katibu wa Afya wa hospitali hiyo, Lucy Sozigwa.
 Mmoja wa wafanyakazi wa benki ya NBC, Ali Lwano,  akigawa sabuni kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, wakati wa hafla hiyo fupi ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na kushiriki shughuli za usafi hospitalini hapo.
 Wafanyakazi wa benki ya NBC, Janeth Mutahanamilwa (katikati) na Emmanuel Mseti (kulia kwake) wakigawa sabuni kwa baadhi ya wagonjwa na watoto wao waliolazwa katika Hospitali ya Temeke.
  Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wa Kanda ya Ilala wakisafisha mazingira ya hospitali hiyo wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wa Kanda ya Ilala na watumishi wa Hospitali ya Temeke wakipozi kwa picha katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na  kushiriki shughuli za usafi hospitalini hapo Dar es Salaam jana. Matawi yaliyoshiriki katika hafla hiyo ni,  hiyo Corporate, Mnazi Mmoja, Kichwele, Samora, Industrial, Kariakoo, Muhimbili, Chang’ombe na Mbagala.

No comments: