Tuesday, April 10, 2012

Wateja Vodacom kufurahia kupokea bure simu wawapo safarini Afrika Mashariki na Afrika Kusini.Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania sasa wanaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha katika matumizi ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaposafiri katika nchi tisa za Afrika ambapo Vodacom na wabia wake kibiashara wanatoa huduma.

Nchi hizo na mitandao ya makampuni ya simu katika mabano ni Afrika Kusini (Vodacom), Msumbiji (Vodacom),Lesotho (Vodacom), DRC Congo(Vodacom), Ghana(Vodafone), Kenya (Safaricom), Rwanda (MTN), Uganda (MTN), Uganda (UTL) na Burundi (UCOM).

 Kupitia mitandao ya mawasiliano ya makampuni hayo mteja wa Vodacom Tanzania sasa anaweza kupokea simu BURE, kupokea BURE ujumbe mfupi wa maneno - SMS, kupiga simu na kutumia huduma za Intaneti kwa gharama nafuu anapokuwa safarini katika nchi hizo.
 
Akizungumzia huduma hiyo mpya ya Africa Roaming, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza amesema “Tunajua kwamba watu wanapenda kuwa katika mawasiliano wakati wote bila kujali kama yupo nyumbani Tanzania ama mapumzikoni Afrika Kusini, au katika safari ya kikazi nchini Ghana, bila kuwa na hofu ya gharama za kuunganishwa kimawasiliano safarini - roaming.”

“Tunachokizundua leo ni suluhisho kuwapa wateja wetu utulivu wa mawazo wanaposafiri” Gharama ya matumizi ya Intaneti kwa mteja anapokuwa safarini ni za juu kwa mitandao mingi ya ya simu, leo tunajivunia kuja na gharama nafuu za matumizi ya Intaneti pamoja na za simu na za ujumbe mfupi wa maneno – SMS pindi mteja anapokuwa safarini katika moja ya nchi zilizo katika huduma hii ya African Family.” Aliongeza Bw. Meza

“Huduma hii pamoja na nyenginezo nyingi ambazo Vodacom Tanzania imezizindua hapo kabla zote ni katika kutimiza ahadi yetu ya kubakia kuwa mtandao bora zaidi wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi hapa nchini. Wateja wetu watarajie mengi mazuri zaidi kutoka kwetu katika wiki na hata miezi ijayo.” Amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza

No comments: