Saturday, April 7, 2012

Chadema watangaza kukata Rufaa Mahakama Kuu ya Rufaa Tanzania


VIONGOZI  wa Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamesema wameamua kukataa rufaa dhidi ya hukumu ya Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha iliyotolewa wiki hii ambayo ilimuondoa madarakani Mbunge wa chama hicho Arusha Mjini Godbless Lema.

Rufaa hiyo wanataraji kuikata hivi karibuni katika Mahakama kuu ya Rufaa Tanzania. 
Wakihutubia umati mkubwa wa wakazi wa Arusha na viunga vyake waliofruka katika viwanja vya NMC, mapema leo viongozi hao akiwepo Godbless Lema mwenye aliwasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuondoa hofu na anaimani watashinda.

Mahakama Kuu  Kanda ya Arusha ilitoa hukumu hiyo na kutengeua Ubunge wa Godbless Lema baada ya kumkuta na hatia ya kutumia lugha ya udhalilishaji na maneno ya kashifa dhidi ya mgombea wa  Balozi Dk. Batilda Buriani katika uchaguzi wa mwaka 2010 alipokuwa akigombea kwa tiketi ya CCM.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Freeman Mbowe alisema zipo sababu tatu zilizowafanya waende kukata Rufani badala ya kuingia kwenye uchaguzi mdogo moja kwa moja.

Mbowe alisema kwamba hawawezi kuacha tu bila kukata rufaa na kukimbilia katika uchaguzi mdogo maana kufanya hivyo ni kukubaliana na maamuzi ya kihuni yaliyotolewa ili kuchezea fedha za Watanzania. 

“Tukiingia kwenye uchaguzi mdogo ndugu zangu tutakuwa tunakubali kuwa Lema alishinda kwasababu alidhalilisha wanawake katika jimbo la Arusha, kitendo ambacho sisi hatuamini,” alisema Mbowe .

Akitaja sababu ya pili alisema upo ukweli kuwa Serikali ya CCM imejaa ufisadi hivyo imekuwa haioni gharama za kutumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya chaguzi ndogo. 

Alisema kama wao wakiamua kuingia katika uchaguzi mdogo ni wazi kuwa watakuwa wameruhusu matumizi makubwa ya fedha za wananchi masikini yatumike wakati nafasi ya kukata Rufani walikuwanayo. 

“CCM wanakimbilia kujilipa posho wawapo kwenye uchaguzi mdogo, sasa kwa vile ukitaka Rufani unasubiria majibu mawili, Rufani inaweza kuturudishia mbunge wetu au ikaitupa Rufani yetu hayo ni mamuzi yanayoweza kupatikana huko,” alisema Mbowe.

Mara baada ya kuwasili Lema aliyeingia na uwanjani hapo akiwa na gari yake  Mercedez Benz namba za usajili T776 BNK na upande wa pili akiwa na Mbowe pekee, alizungumza  na halaiki hiyo Lema alisema yeye yupo tayari kupigania haki katika maisha yake kwa wakati wote awapo hai. 

Alisema ana amini kuwa wananchi wa Arusha na maeneo mengine wameumia kwa kitendo dhalimu kilichofanywa na Jaji mmoja kukubali kupindisha ukweli kwa faida ya kundi la watu wachache. 

“Sintaingia kwenye ofisi zao, njooni nyumbani na mahali popote tutakapokutana tutafanya kazi ya wananchi waliotuchagua kwa kura nyingi.Nimevuliwa ubunge kihuni na kwa hira sasa Mungu atachukua uhao wao,” alisema Lema. 

Lema alisisitiza kuwa yeye bado ni mbunge, licha ya kuvuliwa ubunge huo na Jaji lakini ataendelea kufanya kazi. “niwaambie mimi bado ni mbunge wenu na nitaendelea kufanya kazi kama kawaida”. 

Aidha Mbunge huyo aliyevuliwa wadhifa wake na mahakama alisema huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu Lema aliwaambia wananchi hao kwamba katika kipindi atakachokuwa akisubiria uamuzi wa Rufani yake Mahakama ya Rufani Tanzania, atahakikisha moto aliouwasha unasambaa nchi nzima. 

“Nitahakikisha anakula mihogo, kutembea kwa miguu ili nifike nchi nzima, sasa kwa vile wao wamechokoza basi mimi nitahakikisha ninafia porini kama noma cha iwe noma na ndio imeanza ya kuhakikisha nchi inabadilika. 

“Niligombea Ubunge si kwasababu ya kuuza sura kama wabunge wengine wanaosinzia bungeni, niligombea ubunge kwa lengo la kupigani haki kwa kizazi cha leo na kijacho. 

“Sasa Arusha harakati ndio zimeanza kama walifikiria tulikuwa tunataka ubunge kwa imekula kwao, wamenitia hasira na sasa hii nchi inaenda kugeuka.

Kwa upande akizungumzia uamuzi wa kutaka Rufani alisema, huo ni uamuzi sahihi kwani kama asipokata rufani atakuwa ametenda dhambi ya kubariki hukumu bandia kuendelea kubakia kwenye kumbukumbu za Mahakama.

“Kilichoniondoa ubunge ni sheria kuchakachuliwa sasa nisipo kata Rufani nitakuwa nimetenda dhambi kubwa ya kubariki uchakachuaji huo,” alisema Lema.

No comments: