Sunday, April 15, 2012

KOCHA WA NGUMI, SUPER D KUANZISHA MPANGO WA KUSAKA MABONDIA 10 BORA

KOCHA wa Kambi ya Ngumi ya mkoa wa Ilala Kimichezo, Rajabu Mhamila, 'Super D', anatarajia kuanzisha mpango maalum wa kutafuta mabondia 10, bora kwa njia ya mazoezi makali ili kuwaandaa kushiriki mashindano ya 10 bora yatakayoanza Mei 4, mwaka huu, jijini Dar es salaam.

Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com  Supera D alisema kuwa ameamua kuanzisha mpango huo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa mabondia wake na kuwa na pumzi ya kutosha katika mchezo huo na nguvu kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani.

Aidha Super D alisema kuwa mabondia wake watashiriki katika mashindano ya 10 bora yaliyoandaliwa na Kinyogoli Foundation yatakayofanyika May 4.

Alisema kuwa mabondia hao watazichapa katika mapambano ya aina yake yatakaofanyika mwezi ujao katika Ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

“Nimeanzisha programu ya aina yake kwa ajili ya kuwajengea uwezo mabondia wangu ili waweze kuwa na pumzi za kutosha katika mashindano mbalimbali” alisema. Super D

Aidha aliongeza kuwa wanaomba wadhamini kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha mchezo huo wa masumbwi kwa kuwapatia vijana zawadi za motisha ili kuwatia moyo kaatika  mashindano hayo yatakayowashirikisha vijana mbalimbali katika uzito
tofauti yatakuwa na lengo la kuendeleza mchezo wa masumbwi Nchini

No comments: