Monday, April 9, 2012

Mashabiki Simba, Yanga wazoa fedha za Push Mobile, Huku wakiwa na furaha


Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala (Kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bahati nasibu ya Push Mobile ambayo pia uwahusisha mashabiki wa klabu ya Yanga. kushoto ni Meneja kampeni wa Push Mobile, Talib Rashid.

MASHABIKI  watano wa klabu kongwe nchini, Simba na Yanga wamejizolea zawadi ya sh. 50,000 kila mmoja katika bahati nasibu ya loyalty SMS campaigns kwa mwaka 2012 inayozihusisha timu hizo mbili.
Meneja kamapeni wa bahati nasibu hiyo, Talib Rashid aliwataja washindi hao kuwa ni Warda Salmin wa Morogoro ambaye ni shabiki wa klabu ya Simba na Athumani Hassan wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni shabiki wa klabu ya Yanga.
Rashid aliwataja mashabiki wengine kuwa ni  Zawadi Sanga (Njombe) na Bruno Changa kutoka Tanga ambao ni mashabiki wa Simba. Pia yumo Peter Msangi kutoka Ilala jijini ambaye ni shabiki wa Yanga.
Mashabiki wa hao walituma neno Simba au Yanga kwenda namba 15678 na kujibu maswali mbali mbali kuhusiana na klabu zao na hatimaye kushinda. Alisema kuwa mbali ya kupewa kitita cha sh. 50,000 kila mmoja, mashabiki hao pia wataingia katika droo  kubwa ambazo washindi watapata pikipiki zenye thamani y ash. Milioni 1.5 kila moja na bajaj yenye thamani ya sh. Milioni 6.
Alisema kuwa kampuni yao itaendelea kutoa zawadi ya sh. 50,000 kwa kila siku kwa muda wa siku 90 na kuwaomba mashabiki wa timu hizo mbili kuendelea kushiriki katika bahati nasibu hiyo.
“Lengo ni kuwazawadia mashabiki wa timu hizi kubwa, lakini kwa kujua undani wa historia ya timu zao kwa kujibu maswali na kuongeza ufahamu, nawaomba washiriki ili waweze kushinda fedha, pikipiki na bajaj,” alisema Rashid.

No comments: