Monday, April 9, 2012

WAZIRI WA MAMBO YA NJE MH. MEMBE AHUZUNIKA NA JUU YA KIFO CHA MSANII KANUMBA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amemlilia Muigizaji Steven Kanumba kama Muigizaji maarufu aliyeitangaza Tanzania katika medani za kimataifa ambaye uhai wake umekatishwa ghafla. 

Akizungumza katika Tamasha la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jana, Mhe. Waziri Membe, huku akishangiliwa na Umati wa watu alisema tasnia ya sanaa imepata msiba mkubwa kwa kupotelewa na Mwigizaji Steven Kanumba kufuatia kifo cha ghafla kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 8 Aprili,2012. 

"Nimestushwa sana na msiba huo mkubwa. Kanumba alikuwa Balozi wetu mkubwa nje, umaarufu wake ulifika hata ambako nchi yetu haina Ubalozi, na kupitia uigizaje wake, ameweza kuwa mgeni wa familia nyingi kwenye sebule zao kupitia luningani. Naomba tusimame dakika moja tumuombee na kumtakia heri." alisema Waziri Membe. 


No comments: