Monday, April 16, 2012

Rais Jakaya Kikwete Aomboleza Kifo Cha Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Young Africans Sports Club Bw. 'Ruta'

 Mjumbe  wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Wakili Theonist Rutashoborwa
--
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti  wa klabu ya mpira wa miguu ya Young Africans Sports Club (Yanga)  Bw. Lyod Nchunga kufuatia kifo cha Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, wakili Theonist Rutashoborwa (pichani), aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.


“Nimepokea kwa Masikitiko na huzuni sana taarifa za wakili Theonist Rutashoborwa kilichotokea usiku wa Kuamkia leo, hili ni pigo na pengo kubwa katika klabu ya Yanga katika kipindi hiki cha kushiriki ligi kuu” Rais amesema.


“Naomba unifikishie rambirambi zangu za dhati kwa familia, wachezaji na wana Yanga wote kwa kuondokewa na Mjumbe wao katika kipindi hiki” Rais ameongeza na kuwataka wana Yanga wawe wavumilivu wakati wa msiba huu na kumuombea Bw. Rutashoborwa mapumziko mema ya Milele.

                                                                                                  Imetolewa na

                                                                         Premi Kibanga,
                                                   Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
                                                                      Ikulu-Dar-Es-Salaam
                                                                         12 April, 2012

No comments: