Wednesday, April 11, 2012

RAIS KIKWETE AMTEUA MAKAMU WAKE DKT BILAL KUWA MKUU WA CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA CHA NELSON MANDELA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo, Jumatano, Aprili 11, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema Rais Kikwete pia amemteua Profesa David Homeli Mwakyusa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha chuo hicho cha Nelson Mandela.
Taarifa imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Bilal ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Profesa Mwakyusa aliyepata kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika Serikali ya Rais Kikwete ulianza Alhamisi iliyopita, Aprili 5, 2012.
Chuo cha Nelson Mandela ambacho kiko Arusha ni moja ya vyuo vikuu vinne vinavyolenga kuendeleza sayansi na teknolojia katika Bara la Afrika.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
11 Aprili, 2012

No comments: