Lissu apangua hoja za CCM kwa masaa 3 na nusu (3:30) : kauli ya mwisho anayosema ni kuwa katika tuhuma zote zilizoletwa mahakamani, hakuna ushahidi hata mmoja wa mawakala wa CCM, au wapiga kura wa CCM waliolalamika kuwa kulikuwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.
Hakuna hata wakala mmoja wa CCM aliyejaza fomu namba 14 ya kutoridhika na upigaji kura. Sheria za uchaguzi zinasema wakala ajaze fomu kuonyesha kuwa ameridhika au hajaridhika na kulalamikia tuhuma iliyoletwa mahakamani.
Jambo la pili Hakuna wakala hata moja aliyejaza fomu namba 16 ambaye hakuridhika na zoezi la kuhesabu kura na kutangaza matokeo
Tatu: Hakuna ushahidi wowote wa nyaraka, kuonyesha kuwa CCM au mgombea wao wa Ubunge, au diwani, au wakala wao aliyelalamika kwenye kamati ya maadili ya uchaguzi ya Jimbo la Singida mashariki, au kwa jambo lolote lile.
Na hakuna ushahidi wowote uliotolewa wa malalamiko yeyote. Ushahidi uliotolewa wa Bw. Robert Kimanda, anadai kuwa aliwahi kusema kuwa alijaza. Lakini shahidi aliyefuata alisema kuwa baada yakugundua kuwa CCM wameshinda katika kituo alichosimamia, aliichana fomu hiyo. Kuna malalamiko mengi lakini mengi yanatokana na umbumbumbu wa kutojua sheria za uchaguzi.
Kutokuwepo kwa malalamiko kunaonyesha kuwa hakukuwepo tatizo, kesi imetengenezwa baadaye na watu walioshindwa kwenye uchaguzi. Mheshimiwa jaji, Mashahidi walipingana, wengine walisema walioleta mashataka ni waongo.
Kama mashahidi wa upande wa walalamikaji wanaitana waongo mheshimiwa jaji, kuna nini chakuongeza? Shahidi namba 16, alisema waleta maombi ni waongo.
Kwa hisani ya Josephat Isango
Habari kwa hisani ya Mjengwa Blog
No comments:
Post a Comment