Saturday, April 14, 2012

TBL WADHAMINI WAPYA TAIFA STARS

BIA ya Kilimanjaro Premeum Lager
rasmi ndio mdhamini mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars,
bongostaz imeipata hiyo.
Bia hiyo inayozalishwa na kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), wiki hii itafanya hafa maalum ya kuutangaza rasmi
udhamini huo.
Chanzo cha habari kutoka TBL,
kimesema hafla hiyo itafanyikia katika hoteli ya Serena, iliyokuwa Royal Palm Movenpick,
Dar es Salaam wiki hii.   
Tangu mwaka 2006, Taifa Stars
imekuwa ikidhaminiwa na Serengeti Breweries Limited ambao wameshindwa kuingia
mkataba mpya na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa sababu ya kupandishiwa
dau.  
Baada ya mkataba wao (SBL) kufikia tamati Desemba, mwaka
jana, TFF ikaipandishia dau la udhamini kutoka Sh. Bilioni 1.2 hadi Bilioni
3.6, ambayo ni zaidi ya asilimia 300.


TBL imekubali kuidhamini Stars kwa dau la Sh. Bilioni 3.6
kwa mwaka.
Kilimanjaro pia ni
wadhamini wa watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga na
mashindano ya Kombe la Taifa, Kili Taifa Cup.

No comments: