Monday, April 9, 2012

UZINDUZI WA MISS TABATA 2012 WAFANA VILIVYO.


Warembo wa wanaoshiriki shindano la kumsakama Malkia wa Tabata 2012 wakipozi mbele ya mashabiki wa burudani ya urembo jijini Dar es Salaam waliohudhuria uzinduzi wa shindano hilo la Urembo katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jana. Picha Zote na Father Kidevu Blog.
 Warembo wakicheza Show maalum ya utambulisho wao. Goma la Don’t Take My Number ndio liliwaongoza.
 Mwimbaji mkongwe asiyechoka wala kuzeeka, Mumin Mwijuma akikamua na kundi lake la Twanga Pepeta.
 Shabiki mkubwa wa Twanga, Tomm Chilala akiyarudi magoma na mdau mwenzake.
Wadau wa Burudani na Urembo wakifatilia burudani na uzinduzi huo ulioletwa na Bob Interteinment na kudhaminiwa na Konyagi na Dodoma Wine.
Wadau mbalimbali wa Burudani na Urembo walihudhuria katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na Show kali kutoka kwao Twanga Pepeta “Kisima cha Burudani” na Mashauzi Clasic Modern Taarab kutoka kwake Mtoto wa Kikurya Aisha Ramadhani  ‘Mashauzi’. 
Picha na Father Kidevu Blog.

No comments: