Tuesday, April 17, 2012

Wakazi 400 Dar wajihifadhi CCM

Wakazi 400 wa Magomeni Suna, na Makanya, jijini Dar es Salaam, wamejihifadhi kwenye viwanja vya Ofisi za CCM  Kata ya Magomeni baada ya nyumba zao kujaa maji, kufuatia mvua zilizonyesha wiki iliyopita.
Wakazi hao walisema wamelazimika kujihifadhi kwenye ofisi hizo kwa kuwa hawana sehemu nyingine ya kukimbilia.

Khalid Mtambo, alisema wapo eneo hilo toka Jumatano,  lakini mpaka sasa hakuna msaada wowote wanaoupata toka serikalini licha ya viongozi wa wilaya pamoja na mkoa kuwatembelea na kuwaahidi kuwapa msaada wa chakula.
Naye Anna Ngonyani aliiomba serikali, watu binafsi na taasisi kuwasaidia vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula, mahema.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Fortnatus Fwema, alisema wenye mafuriko Disemba mwaka jana, waathirika wa mafuriko waligawanywa kwenye makundi mawili, ambayo ni wale ambao hawakuwa na nyumba, ambao walipelekwa kwenye makambi, na baadaye Mabwepande.
Fwema alisema kundi la pili ni wale waliokuwa ni wenye nyumba ambao wengine walikwenda kwenye makambi na kuhamishiwa Mabwepande, na wengine waliamua kujihifadhi kwa ndugu na jamaa zao, na wengine waliamua kurudi kwenye nyumba zao.
Alisema kuwa  ambao wamejikusanya pale ndio hao ambao Serikali ilipanga kuwapa viwanja katika zoezi lanalofuata, na kutokana na orodha aliyonayo ni watu 217 tu kwa Wilaya ya Kinondoni.
CHANZO: NIPASHE

No comments: