Tuesday, April 17, 2012

WASHINDI WA KILIMANJARO MUSIC AWARD KUFANYA ZIARA MIKOANI


Meneja wa kinywaji cha bia cha Kilimanaro Lager akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Savannah Lounge jijini Dar es salaam kuhusua ziara ya washindi wa tuzo za Kilimanjaro Music Award, Katikati ni mwanamuziki Diamond na kushoto ni Mwakilishi wa EATV Olympia  Franteu.
 
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa Kilimanjaro Music Awards leo wamezindua rasmi ziara ya washindi wa tuzo hizi kwa mwaka 2012.

Ziara hizi zitakazofanyika katika mikoa 6 ya Tanzânia zitahusisha uvumbuzi wa vipaji vichanga vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya. Mikoa itakayohusishwa ni Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara na kilele kuwa Dar es Salaam.
Ziara hii ya aina yae itajumuisha wasanii walioshinda tuzo za muziki za Kili, na hão watakaozinduliwa kwenye mikoa husika na kuwapa nafasi wasanii hão chipukizi kushiriki kikamilifu na kuonyesha vipaji vyao kama mpango wa bia ya Kilimanjaro wa kuzindua vipaji.

“Tunataka kuondoa mawazo hasi yaliyopo kwamba Tuzo za muziki za Kili ni za Dar es Salaam tu. Mwaka huu bali na kuwapeleka washindi wa tuzo mikoani tumeamua pia kuzindua vipaji vipya kweye mikoa hiyo kwani tunaamini kuwa vipaji vya muziki vinapatikana Tanzânia nzima. 
Vilevile tutawapa nafasi wasaniii watakaovumbuliwa kuimba na washindi vinara wa tuzo za Kili ambapo mshindi mmoja wa kila mkoa ataletwa Dar es Salaam kushiriki kwenye tamasha la mwisho la ziara, na pia kurekodiwa nyimbo moja ya kumwezesha kuanza safari yake ya muziki.” Alisema George Kavishe meneja masoko wa  bia ya Kilimanjaro.

Kati ya wasanii watakaoshiriki kwenye ziara hizi za washindi wa tuzo za Kili ni pamoja na Diamond, Khadija Kopa, Suma Lee, Warriours from the East, Ali Kiba, AT, Aisha Msharuzi, Twanga Pepeta, Ben Pol, Roma, Ommy Dimples, Kalijo Kitokololo, Jaguar na Barnaba
Msanii mahiri Diamond ambaye amejinyakulia tuzo 3 kwenye tuzo za Kili wiki iliyopita alisema “Nina furaha kubwa kuwa kati ya washiriki wa ziara hizi, ni nafasi ya kipekee kwa mimi kukutana na mashabiki wangu walioko mikoani na kuwaonyesha shukurani zangu kwa upendo wao kwangu” Mbali na ziara hii kutegemea kuongeza mshikamano wa watanzania kwenye kushabikia muziki wa ndani pia itaongeza msisimko wa watanzania kushabikia wasanii wetu mahiri.
Ziara za tamasha zitaaza mkoani Dodoma tarehe 28 Aprili (Jamuhuri Stadium),  -  Mwanza tarehe 5 Mei (CCM Kirumba), Kiliman

No comments: