Wednesday, May 23, 2012

CHADEMA:Taarifa Rasmi Kwa Umma Kuhusu Kutupiliwa Mbali Kwa Kesi Dhidi ya Mbunge Wa Viti Maalum(CHADEMA)Leticia Nyerere Nchini Marekani

 John Mnyika (Mb)Mkurugenzi wa Habari na Uenezi na Mbunge wa Ubungo CHADEMA
--
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea nakala ya hukumu ya kesi mbili zilizofunguliwa Marekani dhidi ya mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere (CHADEMA) zenye kuonyesha mahakama imetupilia mbali kesi hizo. (Rejea Kiambatanisho).
 
Kwa mujibu wa mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere waliofungua kesi hiyo waliingia mitini baada ya kubainika kwa tuhuma kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya kutengenezwa kwa malengo ya kumchafua hali ambayo ingeweza kuwatia hatiani wahusika kwa kuwasilisha madai ya uongo.
 
Pamoja na kutupiliwa mbali kwa kesi hizo mamlaka husika za Marekani zinaendelea na uchunguzi wa kumsaka aliyetoa madai kwamba Mbunge Leticia Nyerere amekamatwa na kutaka wananchi wamchangie fedha kwenye akaunti iliyotajwa katika ujumbe uliosambazwa kwa njia ya mtandao.
 
Hukumu hii inadhihirisha tahadhari niliyoitoa kwa wanahabari tarehe 17 Mei 2012 ya kuwataka kusubiri maelezo rasmi kutoka kwa Leticia Nyerere na yatokanayo mahakamani kutokana na tuhuma zilizosambazwa kwenye mitandao kuwa na mwelekeo wa siasa chafu kukwaza jitahada zake na  viongozi wa CHADEMA kutokana na kazi walizozifanya za kuwezesha watanzania waishio Marekani kuunga mkono mabadiliko.
 
Chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu suala hili na taarifa zaidi zitatolewa kwa umma katika hatua za baadaye kadiri iwezekanavyo.
 
Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia fursa hii kuwakumbusha watanzania wanaoishi nchini Marekani kuhudhuria kwa wingi katika Mkutano wa CHADEMA utakaofanyika Maryland tarehe 27 Mei 2012 na kuwasiliana na Leticia Nyerere kupitia leticianyerere@rocketmail.com kwa maelezo zaidi.
 
 
Imetolewa


 Tarehe 13 Mei 2012 na:
  


  John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
---
 Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA)Leticia Nyerere


--


*Soma nakala ya hukumu ya kesi mbili zilizofunguliwa Marekani dhidi ya mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere (CHADEMA) zenye kuonyesha mahakama imetupilia mbali kesi hizo. (Rejea Kiambatanisho Hapo Chini).



No comments: