Saturday, May 5, 2012

Mawaziri, hakuna sherehe, nendeni mkawajibike!


Juhudi za kurejesha misingi ya uwajibikaji katikautumishi wa umma zimeanza kuzaa matunda Baada ya Rais kutekeleza shinikizo laBunge la kuwafukuza kazi baadhi ya Mawaziri ambao Wizara zao zimetuhumiwa kwaubadhirifu wa fedha za umma, rushwa na utendaji mbovu. Mawaziri 6 wamefukuzwakazi baada ya kugoma kujiuzulu wao wenyewe, manaibu Waziri 2 wamefukuzwa pia. 

Ndugu George Mkuchika alitakiwa kujiuzulu, akajiuzululakini Rais amemrudisha kwenye Baraza Kama Waziri wa Utawala Bora. Yeyenampongeza kwani hakuwa na makuu ya kuanza kujitetea Kama wengine. Atakuwaametoa funzo kwa wenzake.

Kwa kawaida wateule hufanya sherehe kwa kuteuliwa kwao.Nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia.Nitawashangaa Watakaokwenda kuapa na Maua kwa furaha kwani furaha itakuwa yamuda mfupi tu. Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na Wateule wotewatakuwa kikaangoni. Too short honeymoon.

Hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi in changamotonyingi sana. Changamoto ya kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza kwawananchi wengi, changamoto ya kukuza uchumi wa vijijini na kukuza uzalishajiviwandani ili kutengeneza ajira kwa vijana, changamoto ya kuongeza mapato yaUtalii kutoka katika hifadhi zetu na kuvutia watalii zaidi katika nchi yetu.

Nimewapigia simu wateule wengi na kuwaambia, siwapipongezi Bali nawatakia kazi njema. Nawatakia uwajibikaji mwema. Uwajibikajindio msingi wa kupambana na rushwa, uvivu na uzembe. 



Kwa Waziri wa Fedha, ambaye mimi ni Waziri Kivuli wake(Kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni hataniwajibisha pia), namwambia uteuzi wakeni changamoto kubwa sana katika maisha yake.

Hivi sasa eneo lenye Bajeti kubwa kuliko zote nchini nihuduma kwa Deni la Taifa (services to national debt). Lazima kuangalia upyaDeni la Taifa. Hivi sasa Deni la Taifa ukijumlisha na Dhamana za Serikali(government guarantees) limefikia tshs 22trn mpaka Desemba 2011. Nimewahikutaka ukaguzi Maalumu katika 'account' ya Deni la Taifa. Linarejea wigo huu.Tunalipa takribani 1.9trn tshs kwa mwaka kuhudumia Deni la Taifa. Zaidi yaBajeti ya miumbombinu, Afya, Maji, Umeme nk.

Mfumuko wa Bei, misamaha ya kodi na kodi zinazozuiawatanzania kujiajiri ni changamoto kubwa sana Wizara ya Fedha lazima ihangaikenayo.

Usimamizi wa Mashirika ya Umma kupitia Ofisi ya Msajiliwa Hazina na hasa usimamizi wa Hisa za Serikali katika kampuni binafsi nimasuala yanayohitaji masuluhisho sasa na sio baadaye.

 wa Mwalimu wangu dkt. Mwakyembe, utakumbukwa kwa Jambomoja tu. RELI. 'make Railways system work'. Hutakuwa na 'legacy' nyingineisipokuwa Reli maaana Bandari bila Reli ni sawa na Bure. 

Tunatumia zaidi ya tshs 300bn kwa mwaka kukarabatibarabara wakati tunahitaji tshs 200bn kukarabati Reli iweze kusafirisha mzigokwenda Bandarini na kukupa Bandarini.

Ndio maana nasema hakuna Jambo la kusherehekea maanawajibu mliopewa na Rais ni mtihani mkubwa kwenu katika kukitumikia Taifa letu.Msipowajibika, mtakumbwa na fagio la chuma!

Mkisha kula kiapo, kimbieni kazini. Nothing to celebrate.Hit the ground running.

1 comment:

mafuru said...

Ni ujumbe Sahihi kabisa. Nchi ipo pabaya sana. Na vijana wanaounda asilimia kubwa ya idadi ya watanzania wako katika hali mbaya na ya kukata tamaa. Tuna fursa nzuri sana kuliko nchi nyingi sana za kiafrika ambazo zimetupita. Lakini SERIKALI yetu imekuwa hodari kwa safari za KUJIFUNZA na wakiwa nchi hizo za watu HUTOA sifa kemkem bila aibu ya kuona sisi tumeshindwa. Ni aibu