Friday, May 4, 2012

MFUMUKO WA VYAMA VINGI NI SABABU YA KUPOROMOKA KWA UCHUMI WA NCHI:MCHUNGAJI KALATA

Wananchi wakiwa katika moja ya mkutano wa kisiasa
NA MWANDISHI WETU
MFUMUKO wa vyama vingi vya siasa umebainika kuwa ni sababu kubwa
iliyosababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi.
Mwito
huo umetolewa na Mchungaji Christosiler Kalata wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri(KKKT),Usharika wa Matumbi jijini Dar es Salaam leo.
Alisema
kuwa vyama hivyo vimekuwa vikitumika
kama chachu ya kukwamisha kasi ya
maendeleo ya nchi hasa kwa kujiendesha kibinafsi,ikiwa ni pamoja na
kukata tamaa, jambo linaloashiria ufinyu wa maendeleo ya wananchi.
Vile
vile alihoji kuwa ikiwa serikali iliziruhusu taasisi mbalimbali kuanzisha
vyuo,kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya vijana kwa lengo la kupata wataalamu,
badala yake  elimu hiyo wanaitumia
kwa kushikilia madaraka kibinafsi.
“Hatari ninayoiona, ubinafsi umetawala, uchoyo, uvivu, tamaa ya
kutajirika haraka, kazi za mikono ziko wapi? Leo Maprofesa wamekata tamaa,
siasa sasa hivi imekuwa rungu la mwisho la kuiua nchi”.
Alieleza kuwa endapo
wataalamu hao wangetumia vema elimu wanayoipata ingeweza kusaidia katika
sekta mbalimbali hususan katika kubuni bidhaa zenye nembo ya Tanzania.
“Kinachotokea sasa tanzania ni nini? Hakuna ubunifu bali
tunashuhudia maneno yasiyo na vitendo, na wengine wameona siasa ndiyo ajira
yao, na kuamua kuingia huku, tena wakitukanana baina yao na wengine kwa
kuneneana maneno mabaya huku kila mmoja akipigania ajira yake.
Aidha, alichanganua kuwa licha ya serikali kuingia katika
mikataba mbalimbali na nchi za nje lakini mikataba hiyo imekuwa ni sababu ya
kubadilisha mifumo ya nchi na kuingia katika mifumo yao hasa wa vyama vingi vya
siasa.
Mchungaji Kalata anafafanua kwamba mmongo’onyoko huo
umesababisha maafa katika demokrasia, hasa kwa kukosa muongozo wa kulinda
rasilimali za nchi.

No comments: