Wednesday, August 10, 2011

ABIRIA AFIKISHWA KITUO CHA POLISI MKOANI MBEYA

Mtuhumiwa Musa Shabani amefikishwa kituo cha polisi kikuu mkoani Mbeya na kufunguliwa shitaka la Uvunjifu wa amani ndani ya daladala pamoja na kuhatarisha usalama wa abiria wengine.

Dereva wa daladala hiyo Emmanuel Mwaifwani amesema chanzo ugomvi mtuhumiwa huyo ambaye alionekana amelewa majira ya Asubuhi huku akidai kapitilizwa kituo ambapo alitakiwa kushushwa kituo cha Stereo na badala yake akashushwa Fine hali iliyoibua mtafaruku kati yao.

Nao baadhi ya abiria wa daladala hiyo wamekemea tabia iliyofanywa na abiria huyo kwa kusema kuwa madereva na makondakta wanastahili kuheshimiwa kama wafanyakazi wengine.

No comments: