Tuesday, August 9, 2011

WABUNGE WAIWASHIA MOTO SERIKALI JUU YA TATIZO LA WAUZAJI WA MAFUTA NCHINI KUGOMA NA KUSABABISHA ADHA KUBWA KWA WANANCHI


Mwenyekiti
wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba akitoa hoja yake binafsi
ya dharura kuhusu tatizo la mafuta ya petroli nchini na ameitaka
serikali kutoa tamko rasmi jinsi ya kumaliza tatizo hili ambapo wananchi
wengi nchini wanapata taabu kuhusu usafiri katika maeneo mbalimbali.

Mbunge
wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela akichangia Bungeni kuhusu
tatizo la suala la mafuta kufuatia hoja ya dharura aliyoitoa Bungeni leo
Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madinim January Makamba kuhusu
tatizo la mafuta nchini.

Baadhi
ya wabunge wakiunga mkono hoja ya dharura alioyoitoa Mwenyekiti wa
Kamati ya Nishati na Madini Januari Makamba kuhusu tatizi la mafuta
nchini.

Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto (Chadema) akichangia kuhusu sula la
matatizo ya mafuta Bungeni leo ambapo ametaka serikali iwachukulie hatua
wafanyabiashara watakaokuwa wakaidi kutii amri ya serikali kuhusu uzaji
wa nishati ya mafuta.

Waziri
wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) pamoja na Naibu wake,
Adamu Malima (kulia) wakiteta ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini
Dodoma.

Waziri
wa Viwanda na Biashara na Masoko, Dk. Cyril Chami (kushoto) akiteta na
Naibu Waziri wake, Lazaro Nyalandu kabla ya kusoma Bajeti ya Wizara ya
Viwanda Biashara na Masoko kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa
mwaka wa fedha 2011/2012 leo Bungeni Dodoma. 

PICHA ZOTE/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO


No comments: