Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akifunga mlango wa gari lililobeba jeneza (pichani)lenye mwili wa Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayunga, uliokuwa ukisafirishwa leo kutoka Uwanja wa Ndege wa Jeshi, Ukonga kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam.
Juliana Mayunga ambaye ni mjane wa Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), marehemu, Silas Mayunga, akifarijiwa alipokuwa akilia baada ya mwili wa mumewe kuwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege za Jeshi, Dar es Salaam.Mayunga alifariki Jumamosi iliyopita akiwa kwenye matibabu nchini India. Mwili wa Luteni Jenerali Mayunga unatarajiwa kuagwa kesho katika Kambi ya Jeshi ya Lugalo na baadaye nyumbani kwake Shariff Shamba, Ilala, Dar es Salaam.
Picha Zote na Mdau Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment