
Habari zinasema meli ya Sea Bus imekwama katika bahari ya Hindi wakati ikitokea Pemba. Imekwama katika eneo hilo kwa zaidi ya masaa manne sasa.Habari kutoka eneo la tukio zinadai kuwa kukwama kwa meli hiyo kumesababishwa na injini ya meli hiyo kuzimika ghafla katika eneo hilo ambalo ni eneo lenye mkondo mkali na kina kirefu zaidi wa bahari.Baadhi ya abiria waliozungumza wamedai kuwa hadi sasa hali ya taharuki imeendelea kujitokeza katika meli hiyo huku mawimbi makali yakendelea kuipiga meli hiyo.
No comments:
Post a Comment