Thursday, September 15, 2011

KCB Tanzania yatoa msaada wa vifaa kwa Hospitali ya Nyamagana wenye thamani ya Milioni 4.9

 Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Joseph Batholomeo  (Kushoto),  akipokea moja ya vifaa kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya KCB Tanzania Mwanza  Walter Lema. Baadhi ya  vifaa vilivyotolewa na benki hiyo vyenye thamani ya Milioni 4.9/- ni vitanda vya kujifungulia, mashine tano za kupima joto ikiwemo mashine mbili za kupima ujauzito.
 Meneja wa KCB Tanzania Tawi la Mwanza Walter Lema, akimkabidhi Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, Joseph Batholomeo sehemu ya vifaa vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya wodi ya wazazi vyenye thamani ya Milioni 4.9/-. Anayeshuhudia  nyuma yao ni Meneja Mikopo wa KCB Tanzania Baguma Kifumbe.
 Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya Jijini Mwanza , Joseph Batholomeo   akipokea sehemu ya magodoro kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya KCB Tanzania Mwanza,  Walter Lema  kwa ajili ya wodi ya wazazi. Baadhi ya vifaa vilivuokabidhiwa vikiwa na thamani  ya Milioni 4.9/- ni vitanda vya kujifungulia, mashine tano za kupima joto ikiwemo mashine mbili za kupima ujauzito.
 Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa na Benki ya KCB Tanzania tawi la Mwanza kwa  Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya Jijini humo ni Vitanda viwili vya kujifungulia, mashine tano za kupima joto, mashine mbili  za kupimia uzito, vitambaa vya kukinga wagonjwa ( usiri) wakati wa kutoa tiba vitatu, magodoro matatu,  ikiwemo makasha matatu ya kuhifadhia uchafu vyote vikiwa na thamani  Milioni 4.9/-.
Meneja Mikopo wa KCB Tanzania tawi la Mwanza  Buguma Kifumbe akitoa maelezo kuhusiana na msaada wa vifaa uliotolewa na benki hiyo kwa hospitali ya Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyoko Butimba  jijini humo. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo.

= = == ==  == =

KCB Tanzania yatoa msaada wa vifaa kwa Hospitali ya Nyamagana
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vya tiba kwa hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, iliyopo Butimba ya jijini Mwanza ili kusaidia akinamama wanaojifungua.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 4,9/- vilikabidhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo na Meneja wa tawi la Mwanza, Walter Lema na kupokekelewa na Mganga Mkuu  Mfawidhi wa hospitali hiyo  Joseph Batholomeo.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Lema alisema KCB Tanzania kwa kuthamini afya za binadamu na wananchi wa Jiji la Mwanza imetoa msaada huo ili kuwezesha kutolewa kwa huduma bora za afya kwa wazazi na wananchi wengine.
Alisema KCB inatambua umuhimu wa huduma za afya na kwamba wananchi kama wadau wa benki hiyo wakipata huduma bora zinazokidhi wataweza kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za uzalishaji na kujiingizia kipato.
“KCB Tanzania  kama chombo cha fedha wadau wetu wakubwa ni wananchi, ambao bila kuwa na afya njema hawawezi kufanya shughuli za uzalishaji, kadhalika hata sisi tutakuwa tumeathirika, msaada huu kwa hospitali hii umelenga kurudisha faida kwa wadau wetu waweze kupata tiba bora na uhakika” alisema Lema
Kutokana na hilo alibainisha kwamba benki hiyo itaendelea kutoa misaada yenye tija kwa hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu yake na kuwezesha madaktari kutoa huduma bora.
Aidha aliwaasa wananchi na watumishi wa hospitali hiyo kujiunga na benki hiyo kwa vile huduma zake zimesambaa katika nchi za Afrika Mashariki ambapo kwa hapa nchini inayo matawi 11.
Kwa upande wake Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo Joseph Batholomeo  mara baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo ni kwa ajili ya wodi ya wazazi alisema kwa kutambua mahitaji ya jamii wanayoihudumia, vifaa hivyo vitaongeza ufanisi wa huduma wanazozitoa.
Alisema utakuwa chachu ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi na ni vema watumishi wa hospitali hiyo wakiwemo madaktari na wauguzi wakajiunga na  benki ya KCB Tanzania kwa kufungua akaunti  ili kuunga mkono juhudi zao za kusaidia jamii kutokana na faida zinazotokana na wateja wa benki hiyo.
Vifaa vilivyotolewa ni Vitanda viwili vya kujifungulia, mashine tano za kupima joto, mashine mbili za kupimia uzito, vitambaa vya kukinga wagonjwa ( usiri) wakati wa kutoa tiba watatu , magodoro matatu, makoti mawili ya watoto wanaozaliwa , makasha tatu ya kuhifadhia uchafu kwa vifaa tiba vilivyokwishatumika, vifaa vya kuzalishia na Aprona tano .Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 4,935,000.

No comments: