Saturday, September 3, 2011

MAADHIMISHO ya miaka 50 ya UHURU YA JWTZ BASE YA ANGA NGERENGERE.

Gwaride la Askari wa JWTZ Base ya Anga ya Ngerengere, wakifanya onesho la namna mazishi ya Askari mwenzao aliyefariki dunia yanavyokuwa upaande wa Kijeshi na kiraia , wakati wa maadhimisho ya siku ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ya kutimiza miaka 47 tangu kuanzishwa kwake Septemba mosi, 1964.
Gwaride la Askari wa JWTZ Base ya Anga ya Ngerengere, la mazishi wakipinga risasi baridi hewani , kuonesha mfano wa namna ya mazishi ya Askari mwenzao aliyefariki dunia yanavyokuwa upaande wa Kijeshi na kiraia , wakati wa maadhimisho ya siku ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ya kutimiza miaka 47 tangu kuanzishwa kwake Septemba mosi, 1964.
Mkuu wa Komandi ya Vikosi vya Anga Base ya Ngerengere,Brigedia Jenerali Joseph Kapwani ( kushoto) akigonganisha glasi na Mkuu wa Wataalamu wa Kijeshi kutoka Jeshi la Anga la Watu wa Jamhuri ya China, hapa nchini, Kanali Mwandamizi , Zhu You Yu ( kati kati) na (kulia ) ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ya kutimiza miaka 47 tangu kuanzishwa kwake Septemba mosi, 1964.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu( wapili kutoka kushoto) akiwa na mweyeji wake Mkuu wa Kamandi ya Base ya Anga Ngerengere, Brigedia Jenerali, Joseph Kapwani ( watatu kutoka kushoto) pamoja na maafisa waandamizi wengine wa base hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu ( wenye suti) akisalimiana na Askari wanafunzi wa chuo cha Kijeshi cha Anga, Base ya Ngerengere.
Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
Kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments: