Thursday, September 8, 2011

Shule Hii; Miaka 50 Baada Ya Uhuru Wetu!






Ndugu zangu,
Kuna mwenzetu baada ya kuona picha hiyo ya kwanza niliyoiingiza juzi, ameniandikia ujumbe kuniuliza kama mtoto huyo alikuwa annaingia darasani au nyumbani. Naam, alitaka kujua kama kweli hiyo ni shule baada ya miaka 50 ya uhuru.

Ufafanuzi wangu;
- Hiyo ni shule ya msingi katika Tanzania yetu ya leo.
- Huyo ni mwanafunzi anayeingia darasani na mbele ni walimu wa shule wanaoingia darasani kufundisha.
- Hao ni wanafunzi darasani
- Hiyo ni nyumba ya Mwalimu Mkuu
- Na shule ina tundu moja la choo.
Ni miaka 50 baada ya Uhuru wetu. Tafakari.
Maggid,
Iringa.

No comments: