Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya advocate nyombi.
=====
Na mwandishi wetu.
Askari namba G.2795 PC Meshaki Urasa wa kitengo cha ufundi Mbeya mwenye umri miaka 28 kabila Mchaga ameuawa kwa kupigwa na vitu butu vinavyosadikiwa kuwa ni Nondo akiwa nyumbani kwake majira ya saa tano za usiku.
Tukio hilo limetokea kata ya Mabatini jijini Mbeya ambapo imeelezwa kuwa askari huyo alivamiwa na watu wanane ambao bado hawajajulikana na kuanza kumpiga hali iliyomsababishia maumivu makali yaliyompelekea kufariki dunia wakati akipewa matibu katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa askari huyo amesafirishwa jana wenda nyumbani kwao mkoani Arusha mara baada ya taratibu kukamilika.
Aidha amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji hayo na waliohusika ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment