Tuesday, September 6, 2011

Makamu Wa Pili Wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Afungua Ofisi Ya Mbunge Kitope


Mtaalamu wa Kilimo cha mbogamboga Bi Salma Marshed akimuonesha shamba darasa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi wakati alipotembelea shamba la mbogamboga la wana ushirika wa mwendo wa Jongoo liliopo kijiji cha Kazole kilichopo ndani ya jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope akimkabidhi mipira ya maji Katibu wa ushirika wa kilimo cha mbogamboga kiitwacho mwendo wa jongoo Bw, Moh,d Amour Kombo mara baada ya kutembelea shamba la wana ushirika hao, na kuwataka waitumie mipira hiyo kwa kilimo cha umwagiliaji.
Mbunge wa jimbo la Kitope na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Mhe Vuai Ali Vuai wakisaini hati za makabidhiano ya jengo la ofisi ya Mbunge wa Kitope wakati wa sherehe ya makabidhiano ya ofisi hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Mhe Vuai Ali Vuai akimkabidhi rasmi jengo la ofisi ya Mbunge wa Kitope Mhe Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa jimbo hilo. Jengo hili limegharimu Sh,milioni 40 zimetolewa na ofisi ya bunge na ujenzi umesimamiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B,
Jengo la ofisi ya mbunge wa jimbo la Kitope.Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais



No comments: