Saturday, September 10, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA MELI ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Ally Amour wakati alipofika kumjulia hali mtoto Said Gerald (6) aliyenusurika katika ajali ya Meli eneo la Nungwi usiku wa kuamkia leo, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Aliyempakata ni mama yake mzazi, Mariam Hemed.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Baada ya hapo Makamu wa Rais alitembelea katika Viwanja vya Maisala na kutembelea shughuli za kiusaidia na kutambua maiti waliopatikana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

1 comment:

BERNARD KOMBA said...

Poleni ndugu nzetu wa Tanzania Visiwani kwa msiba mkubwa uliowapata, lakini hatuna budi kuishinda simanzi ingawa sio kitu rahisi.

Kazi ya Mungu haina makosa, na serikali kwa makusudi iwasaidie wahanga wa tukio kwa hali na mali ili ipate baraka za mola.