Saturday, September 10, 2011

MAMA SALMA KIKWETE ASHIRIKI MATEMBEZI YA UCHANGIAJI FEDHA YA KUSAIDIA MAMA NA MTOTO

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (mwenye suruali nyeupe) pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Barclays nchini Kihara Maina (mwenye suruali ya kadeti) wakishiriki katika matembezi ya kilo meta kumi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuchangisha fedha ya kusaidia Afya ya Mama na Mtoto.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma kikwete akizindua matembezi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia Afya ya mama na mtoto katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (mwenye suruali nyeupe) pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Barclays nchini, Kihara Maina (mwenye suruali ya kadeti) wakishiriki kufanya mazoezi ya viungo na wageni mbali mbali waliohudhulia leo kabla ya kuanza kwa matembezi ya kuchangisha fenda ya kusaidia Mama na Mtoto katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar
washiriki wa matembezi wakipasha misuli moto kabla ya matembezi.Picha na Mwanakombo Jumaa-Maelezo

No comments: