Saturday, September 17, 2011

mtoto agongwa na gari jana maeneo ya Mabibo,Gari lililomgonga lakimbia

Mtoto ambaye hakutambulika jina lake mara moja,anaekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 14-16 akiwa amelala kwenye barabara mara baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Hilux lenye rangi nyeusi,maeneo ya TGNP Mabibo jijini Dar jioni hii.Nambari za usajili za Gari hilo hazikuweza kupatikana mara moja kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa gari hilo mara baada ya kumgonga mtoto huyo ambaye baadae alikimbizwa hospitali kwa matibabu.
Baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kwenye kilele cha Tamasha la 10 la Jinsia lililokuwa limeratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakikimbilia barabarani kumuangalia mtoto aliegongwa na gari jioni ya leo Maeneo ya Mabibo,jijini Dar.
Mmoja wa wasamalia wema akiwa amembeba mtoto huyo kumpeleka kwenye gari tayari kwa safari ya kumuwahisha Hospitali ili aweze kupatika matibabu ya haraka.
Kila mtu alikuwa na Shahuku ya kutaka kumtambua mtoto huyo wakati akiingizwa kwenye gari tayari kwa kumkimbiza hospitali ili aweze kupatika matibabu ya haraka.
PICHA KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

No comments: