NA FRANCIS GODWIN
Wakati tamasha na wanaharakati wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) likiendelea katika viwanja vya mabibo jijini Dar es Salaam na kesho ikiwa ni usiku wa mwanamke wa kiafrika ,mkoani Iringa mwanamke mmoja ambaye jina bado kufahamika amefanya unyama wa kutisha na kushangaza wengi baada ya kujifungua salama watoto wawili mapacha na badala ya kuwatunza amewatupa barabarani na kutoweka.
Mwandishi maalum wa mtandao huu kutoka mkoani Iringa anaripoti kuwa mwanamke huyo alitenda unyama huo jana mchana na kuwa kuwa hadi sasa jitihada za polisi za kumsaka mwanamke huyo zikiwa bado zinaendelea.
Pamoja na wanaharakati mbali mbali kwa nyakati tofauti jana katika tamasha la TGNP kuonyesha kupinga vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya wanawake dhidi ya watoto wanaowazaa ila bado sauti ya wanaharakati hao imeonekana kutowafikia wanawake wachache ama imewafikia ila wameonyesha kuziba masikio yao kwa pamba.
No comments:
Post a Comment