Monday, September 19, 2011

Rais Jakaya Kikwete Aongoza Kikao Cha Maandalizi Ya Mkutano Wa 66 Wa Umoja Wa Mataifa Nchini Marekani

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika hoteli ya Jumeirah Essex House jijini New York Marekani Jumapili tayari kwa mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa,hapa anaonekana katika picha akipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwambata wa Jeshi katika ubalozi wa tanzania umoja wa Mataifa Kanali Wilbert Ibuge.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dkt Rachel Mhaville ambaye ni daktari bingwa wa meno ya watoto.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Bukombe (CHADEMA) Prof. Kulikoyela Kahigi ambaye pamoja na Mbunge wa Liwale (CCM) Mh Faith Mitambo (wa pili kulia) ameongozana nao kuhudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa mataifa
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha maandalizi kwa ajili ya mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa

No comments: