Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akihutubia Mkutano wa Afrika-Asia 2011 leo ambapo amesisitiza elimu yenye maadili ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwanamke pamoja na jamii kwa ujumla. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Wanawake cha Sookmyung nchini Korea Kusini ambacho kimetiza miaka mia moja na tano tangu kianzishwe 1906.
Baadaye Spika Makinda alipata wasaa wa kukutana na vyombo vya habari na kufafanua umuhimu wa kuwa na vyuo vikuu vya wanawake. Hapa anaongena Avivang Tv ya Korea
Salma Dinya ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ambaye alialikwa kwenye mkutano huo kuiwakilisha Tanzania kama kiongozi kijana. Hapa anatoa mada kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Asia na Afrika kuhusu Tanzania.
Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa na mwenyeji wake Dkt Han, Rais wa Chuo Kikuu cha wanawake cha Sookmyung, Korea
Kwa picha na matukio zaidi tembelea www.prince-minja.blogspot.com
No comments:
Post a Comment